Isaiah 54:8-10

8 aKatika ukali wa hasira
nilikuficha uso wangu kwa kitambo,
lakini kwa fadhili za milele
nitakuwa na huruma juu yako,”
asema Bwana Mkombozi wako.

9 b“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa,
nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia.
Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,
kamwe sitawakemea tena.
10 cIjapotikisika milima, na vilima viondolewe,
hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,
wala agano langu la amani halitaondolewa,”
asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.
Copyright information for SwhNEN